Taifa Stars usoni mwa Zambia Nusu fainali COSAFA 2017. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 03, 2017

Taifa Stars usoni mwa Zambia Nusu fainali COSAFA 2017.

Goli pekee la mshambuliaji wa Taifa Stars na klabu ya Dhofar ya Oman Elias Maguri limeiwezesha Stars kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano ya Cosafa 2017.

Taifa Stars imepata ushindi wake wakati ikicheza dhidi ya wenyeji Afrika Kusini ambao ndio walikuwa Mabingwa watetezi wa taji hilo.
Maguri amefunga bao hilo pekee dakika ya 18 kipindi cha kwanza baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa Mazamiru Yassin.

Baada ya mchezo, Maguri alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo baada ya kuonesha kiwango kizuri ikiwa ni pamoja na kufunga goli lililoisaidia Stars kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.

Taifa Stars itacheza na Zambia katika hatua ya nusu fainali baada ya Zambia wao kushinda 2-1 mchezo wao wa robo fainali walipo cheza dhidi ya Botswana.

Mechi ya nusu fainali ya Cosafa kati ya Taifa Stars dhidi ya Zambia itachezwa Julai 5, 2017.

Post Bottom Ad