Kesi ya Aveva na Kaburu yasogezwa mbele hadi Agosti 7. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 31, 2017

Kesi ya Aveva na Kaburu yasogezwa mbele hadi Agosti 7.

Godfrey Nyange ‘Kaburu (mweupe kushoto) na Evans Aveva (mwenye miwani).

Kesi ya madai ya utakatishaji fedha inayowakabili Viongozi wa Simba SC, Rais Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ imeahirishwa kusikilizwa leo Julai 31,2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam , kutokana na upelelezi wake kutokamilika.

Kesi hiyo iliyokuwa isikilizwe na Hakimu Victoria Nongwa imepamgwa kusikilizwa tena Agosti 7,2017 mahakamani hapo, ambapo watuhumiwa wamerudishwa gerezani.

Aveva na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Klabu ya Simba SC na kutakatisha dola 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa rumande tangu Juni 29, mwaka huu.

Post Bottom Ad