Ripoti ya Pili ya Makinikia- Waliotajwa wazuiliwa kutoka nje ya Nchi. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, June 13, 2017

Ripoti ya Pili ya Makinikia- Waliotajwa wazuiliwa kutoka nje ya Nchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  amepokea Taarifa ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo Profesa Nehemiah Osoro, Mapema jana Juni 12.2017,  Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akionesha Ripoti hiyo ya Kamati ya pili ya Uchunguzi wa Madini yaliyo kwenye makontena yenye mchanga unaosafirishwa nje ya nchi kutoka kwenye machimbo ya madini sehemu mbalimbali hapa nchini mara baada ya kukabidhiwa Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na kulia ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakishuhudia.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania, Mwigulu Nchemba.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametoa taarifa ya kumpongeza Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kwa uamuzi aliochukua baada ya kupokea ripoti ya pili ya mchanga wa madini.

Pamoja na pongezi, Waziri Nchemba ametoa maagizo kuwa watu wote waliotajwa kwenye ripoti hiyo wasiruhusiwe kutoka nje ya nchi isipokuwa kwa ruhusa maalum kutoka serikalini na kuvitaka vyombo vya usalama kuhakikisha vinasimamia agizo hilo.

Hakuna uzalendo zaidi ya kulinda rasilimali za Taifa, Hakuna utetezi wa wanyonge zaidi ya kulinda rasilimali zao.Hongera sana Mh.Rais kwa uzalendo wa vitendo kwa Taifa letu.

Naelekeza wote waliotajwa kuhusika hakuna kutoka nje ya mipaka ya nchi yetu isipokuwa kwa kibali maalum kutoka serikalini. Vyombo vitekeleze maagizo ya Rais kwa utimamu,” imesema sehemu ya taarifa ya Mwigulu Nchemba.

Post Bottom Ad