UPDATE-Ajali-Karatu: Watu 32 wapoteza Maisha katika ajali ya Basi. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Saturday, May 06, 2017

UPDATE-Ajali-Karatu: Watu 32 wapoteza Maisha katika ajali ya Basi.


Jumla ya Maiti  32 zimepokelewa katika Hospital ya Lutheran Karatu baada ya basi aina ya Costa lenye namba za usajili T 871 BYS kupata ajali (Pichani) likiwa limewabeba Wanafunzi na Walimu wao wa shule ya St. Lucky Vincent Nursery & English Medium Primary School kisha kutumbukia mtaroni katika eneo la Mlima Rhotia wilayani Karatu Mkoani Arusha wakati wakielekea kwenye ziara ya kimasomo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo akithibitisha tukio hilo amesema ajali hiyo imetokea mapema leo,May 06,2017 baada ya Gari aina ya Toyota Costa yenye namba za usajili T 871 BYS lililokuwa limewabeba Wanafunzi na Walimu wao waliokuwa wakielekea shule ya Msingi Tumaini iliyopo Mjini Karatu , kumshinda dereva na kutumbukia korongoni katika eneo la Rotia jirani kabisa na Mji wa Karatu ambapo waliothibitika kupoteza maisha ni Wanafunzi 29 kati yao Wavulana ni 12 na Wasichana 17,huku Walimu 2 na Dereva wa gari hilo nao wakiripotiwa kupoteza maisha.

Post Bottom Ad