Picha/Ajali-Karatu: Coaster yaua Wanafunzi zaidi ya 20. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, May 06, 2017

Picha/Ajali-Karatu: Coaster yaua Wanafunzi zaidi ya 20.

Wanafunzi zaidi ya 20 na walimu wao (idadi haijafahamika) wamefariki dunia baada ya basi aina ya Coaster waliokuwa wakisafiria kuacha njia na kutumbukia mtaroni katika eneo la Mlima Rhotia wilayani Karatu Mkoani Arusha wakati wakielekea kwenye ziara ya kimasomo.

 Aidha taarifa zaidi zinaeleza kuwa wanafunzi hao ni wa shule ya St. Lucky Vincent Nursery & English Medium Primary School iliyopo Arusha, walikuwa wakienda kwenye shule nyingine kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mtihani wa ujirani mwema.
Inaelezwa kuwa ni watoto wanne(4) pekee ndiyo wanasadikiwa kuwa wako hai ila wako mahututi  na kuna wasi wasi vifo vikaongezeka kutokana na hali mbaya ya majeru wa ajali hiyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Charles Mkumbo amethibitisha na kusema atatoa taarifa kama ajali hiyo imesababisha madhara akifika eneo la tukio.
Taarifa zaidi kukujia baadae.

Hapa Chini ni Baadhi ya Picha toka eneo la tukio.
 Post Bottom Ad