VPL 2016/2017- Yanga SC wakaa kileleni kwa ushindi wa 2-0 huku JKT Ruvu ikishuka Daraja. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Saturday, May 06, 2017

VPL 2016/2017- Yanga SC wakaa kileleni kwa ushindi wa 2-0 huku JKT Ruvu ikishuka Daraja.

Wachezaji wa Yanga SC wakiwa wamewakumbatia wafungaji wa mabao yao, Amissi Joselyn Tambwe  na Obrey Chirwa kuwapongeza.

Timu ya Yanga SC imerudi kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya jioni ya leo May 06,2017 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Pongezi kwa Mrundi, Amissi Joselyn Tambwe aliyefunga bao la kwanza na kuseti la pili lililofungwa na Obrey Chirwa katika mchezo wa leo na sasa Yanga inafikisha pointi 59 baada ya kucheza mechi 26 na japo wanalingana kwa pointi na Simba SC iliyocheza mechi 27, lakini wanakwenda juu kwa wastani wao mzuri wa mabao.
Matokeo ya Mechi nyingine zote za leo VPL 2016/2017.

Aidha ,Timu ya JKT Ruvu imekuwa ya kwanza kushuka daraja katika msimu huu wa ligi kuu Tanzania bara mara baada ya kupoteza mechi yake ya ugenini kwa kipigo cha bao 2-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza.

JKT Ruvu ina pointi 23 baada ya kucheza mechi 28 ikiwa imebakiza mechi mbili pekee kabla ya msimu kumalizika.

Hata kama watashinda mechi zao mbili zilizosalia kwenye ligi, watafikisha pointi 29 ambazo haziwaruhusu kusalia kwenye ligi.

Msimu uliopita timu ya JKT Mgambo ilishuka daraja kwa hiyo kushuka kwa JKT Ruvu kunafanya timu mbili za jeshi la kujenga taifa kushuka daraja ndani ya misimu miwili mfululizo.

Msimamo baada ya Mechi za leo.

Post Bottom Ad