Tumuombeeni Mzee Majuto.! - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 23, 2017

Tumuombeeni Mzee Majuto.!

Mze Majuto akiwa na familia yake.

Tumuombeeni! Lejendari wa vichekesho Bongo, Amri Athman ‘Mzee Majuto’ yu taaban kwa takribani wiki mbili sasa kufuatia kubanwa na ugonjwa wa ngiri huku mkewe, Mama Bilal naye akisumbuliwa na homa, jambo ambalo staa huyo ameomba Watanzania wamuombee.

KUTOKA TANGA

Katika mazungumzo na Mwandishi kwa njia ya simu akiwa nyumbani kwake, Tanga, Mzee Majuto alisema kuwa, ni wiki ya pili sasa hali yake kiafya si nzuri, mara nyingi amekuwa akitumia dawa za hospitali na zile za kienyeji lakini hakuna unafuu wowote anaoupata.

“Nasumbuliwa sana na ngiri, sasa nakwenda wiki ya pili na siku kadhaa, hali si nzuri kabisa na kuna kipindi nililazwa, lakini sikupata nafuu, dawa nimemeza hadi nahisi nina stoo ya madawa tumboni, mama Bilal (mkewe) ambaye ndiye msaidizi na mhudumu wangu, naye anasumbuliwa na homa kali, namlilia Mungu juu ya jambo hili,” alisema Mzee Majuto.

NGIRI NI UGONJWA GANI?

Katika kujiridhisha kwa undani zaidi juu ya ugonjwa huo, Baadhi ya madaktari bingwa ambao kwa nyakati tofauti walitoa ufafanuzi toshelezi juu ya tatizo hilo linalosumbua watu wengi.

Ngiri au hernia ni aina ya ugonjwa ambao unampata mtu baada ya misuli au kuta za tishu mwilini zinazoshikilia au kubeba viungo (organs) fulani kupoteza uimara au kuwa na uwazi (opening) hivyo kusababisha viungo hivyo kutoshikiliwa ipasavyo,” alisema mmoja wa madaktari walioulizwa na Na Mwandishi wa Habari hii na kuongeza:

“Tatizo la ngiri huweza kumpata mtu yeyote. Miongoni mwa vitu vinavyoweza kumsababisha mtu apate ugonjwa wa ngiri ni kuwa na uzito mkubwa au kuongezeka uzito kwa ghafla, kazi ya kubeba au kunyanyua vitu vizito, tatizo la kukohoa au kupiga chafya kwa muda mrefu, ujauzito au matatizo yanayojitokeza kwa mwanamke wakati wa kujifungua. 

Pia kuharisha au kuvimbiwa (constipation). Vitu hivyo humfanya mtu apate ngiri (hernia).


Post Bottom Ad