Tizama Picha 6 za treni ya starehe ilioundwa India. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, May 30, 2017

Tizama Picha 6 za treni ya starehe ilioundwa India.

Treni ya kwanza iliyoundwa Nchini India imeanza kufanya kazi.

Tejas Express ina mabehewa yalio na viti vya starehena burudani ikiwemo filamu za Bollywood zinazoonyeshwa.

Kuna mashine za chakula na vinywaji kama chai na kahawa ndani ya treni.

Treni hiyo pia ina mtandao kupitia WI-Fi, michezo ya kompyuta na pia mtu anaweza kusikiliza matangazo na muziki.

 Treni ya Tejas Express imeanza kazi na husafiri kati ya Mumbai na jimbo la kitalii la Goa na Treni hiyo husafiri kwa saa nane na nusu kufika Goa kutoka Mumbai, hii ikiwa na kasi zaidi kidogo ikilinganishwana na treni nyingine.

Treni hiyo ina milango ya kufunguka wenyewe, otomatiki ni ya kwanza nchini India. Inaweza kwenda kwa mwendo kasi wa kilomita 200 kwa saa, lakini kuna udhibiti wa kasi wa treni nchini.

Inatarajiwa kuhudumu mara tano kwa wiki, kando na wakati wa msimu wa upepo mkali ambako itakuwa ikihudumu mara tatu kwa wiki.

Tiketi za kawaida huuzwa $18; huku za kiwango cha juu ni rupi 2,590.

Iwapo treni hiyo itapata umaarufu maafisa wanapanga kupanua huduma wakianza na jimbo jirani la Gujarat , kwa mujibu wa taarifa.

Post Bottom Ad