Haji Manara-Bingwa halali atatangazwa hivi karibuni. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 30, 2017

Haji Manara-Bingwa halali atatangazwa hivi karibuni.

Haji Manara.

Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Simba SC, Haji Manara ameendelea kusisitiza kuwa klabu hiyo ndio mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara kwa msimu huu kinachosubiriwa sasa ni maamuzi kutoka FIFA kwani ubingwa wao ni wa jasho na damu.

 Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii Manara ameandika, ‘Simba ni Bingwa wa kombe la Shirikisho, ni Bingwa wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu 2016/2017, ndio ni Bingwa wa nchi msimu huu, ni kusubiri tu wenye mpira wao FIFA waturudishie points zetu tatu zilizo wazi kwa kanuni zote ili tutawazwe rasmi kuwa machampioni wa nchi hii.

Yes no way, mchezaji awe na kadi tatu za njano zilizothibitishwa pasina shaka yoyote na ripoti za waamuzi na makamisaa wa michezo husika na bodi ya ligi yenye jukumu halali la kikatiba la uendeshaji na usimamizi wa ligi, kisha eti kwa matakwa ya ajabu ya Shirikisho na kamati yake isiyo na nguvu ya kisheria na kikanuni iipoke points Simba kwa sababu zozote zile, ni kuibaka kanuni ambayo ipo wazi na ni dhulma isiyohitaji touchi kuiona.

INSHAALAH bingwa halali atatangazwa hivi karibuni.Yes ni ubingwa wa Jasho na damu, ni ubingwa uliotafutwa kwa nguvu zote halali na uliomwaga damu za wanasimba walioumia na kupoteza maisha yao katika kuusaka.

Post Bottom Ad