Simba SC Nakutibua Sherehe za Ubingwa wa Yanga SC Ligi kuu Tanzania bara 2016/2017. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, May 21, 2017

Simba SC Nakutibua Sherehe za Ubingwa wa Yanga SC Ligi kuu Tanzania bara 2016/2017.

Baada ya kuenea kwa tetesi kuwa Klabu ya Simba SC imewasilisha malalamiko ya barua kwa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupinga kunyang'anywa pointi 3, hatimaye uthibitisho wapatikana.

Kitendo cha Simba SC kuwasilisha rufaa hiyo na kuenea kwa picha ikionyesha vielelezo hivyo, imeanza kuwakwaza mashabiki wa Yanga SC ambao walikuwa wameanza sherehe za Ubingwa baada ya Kikosi chao kufanikiwa kutetea ubingwa wake wa VPL msimu huu ikiwa ni mara ya tatu mfululizo tangu walipolitwaa taji hilo msimu wa 2014/2015 hadi sasa 2016/2017.

Baadhi ya mashabiki wa Yanga SC, wameonekana kukerwa na jambo hilo huku wakiwakejeli Simba SC kwa kuwaita “Wazee wa pointi za mezani”.

Simba SC imeamua kwenda FIFA kuhakikisha inapata pointi tatu ambazo kama itafanikiwa, basi moja kwa moja itatangazwa kuwa Bingwa Ligi Kuu msimu huu 2016/2017.

Haya ni baadhi ya maneno aliyoandika Msemaji wa Simba SC aliyefungiwa, Haji Manara;....."Last week nilipowapongeza Yanga kwa ushindi na kuwaambia mapambano yanaendelea,sijui kama tulielewana!! Bila shaka sasa mmenielewa, soon tutapewa haki yetu,MWANA KULITAKA,MWANA KULIPEWA"

Halafu akaendelea;........"Hv unadhani FIFA wana figisu guys?kadi tatu za njano ni kukosa game inayofuata tu,no way out!!ukizingatia repoti za mwamuzi na kamisaa na bodi inayosimamia ligi, sasa mjiandae kisaikolojia kulileta kombe kwa magoti! SHUBAMIT"


Post Bottom Ad