Taswira Picha –Ajali yaua Dereva na Kujeruhi Watu 4-Mabawe,Ngara/Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, May 21, 2017

Taswira Picha –Ajali yaua Dereva na Kujeruhi Watu 4-Mabawe,Ngara/Kagera.

Muonekano wa gari likiwa limeharibika vibaya baada ya tukio la ajali ya magari mawili yaliyo gongana uso kwa uso katika eneo la Mkafigiri kata ya Mabawe wilayani Ngara mkoani Kagera May 18, 2017 majira ya saa 5 usiku.


Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Ngara mkoani Kagera Bw. Abedi Maige amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba imesababisha Kifo cha Mtu mmoja ,Majeruhi na uharibifu wa magari yote mawili  akizungumzia ajali hiyo iliyo tokea katika eneo la Mkafigiri kata ya mabawe wilayani Ngara mkoani Kagera.
Ajali hii ililihusisha  gari namba T 738  AEB aina ya Toyota Land Cruiser Mali ya Ngara Oil likiendeshwa na Bw.Said Mikidad ( 37 ) akitokea Kabanga kuelekea Ngara Mjini liligongana na gari lililokuwa likielekea nchini Burundi  lenye namba IT 2904 BRD aina ya Toyota  RV4 na kusababisha kifo cha dereva wake  Ndabashinze Paschal ( 46 )  aliyekuwa akitokea Dar Es Salaam kuelekea nchini Burundi.


Mashuhuda wakilitizama  gari namba T 738  AEB aina ya Toyota Land Cruiser Mali ya Ngara Oil likiendeshwa na Bw.Said Mikidad ( 37 ) akitokea Kabanga kuelekea Ngara Mjini liligongana na gari lililokuwa likielekea nchini Burundi  lenye namba IT 2904 BRD aina ya Toyota  RV4 na kusababisha kifo cha dereva wake  Ndabashinze Paschal ( 46 )  aliyekuwa akitokea Dar Es Salaam kuelekea nchini Burundi.
Bw. Maige amesema ajali hiyo imesababisha majeruhi wanne ambao ni Said Mikidad (37) mwenyeji wa Kabanga,Ngara ( Dereva),Tiberth Selestine ( 27) Afisa Afya Kabanga, Charles Mdoe ( 41 ) Dereva na Antony John ( 47) Mfanyabiashara mkazi wa Dar Es Salaam na wote wamelazwa katika Hospitali ya Nyamiaga wakipatiwa matibabu zaidi.

Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa gari la IT  .


Mashuhuda wakiliangalia gari lililokuwa likielekea nchini Burundi  lenye namba IT 2904 BRD aina ya Toyota  RV4 baada ya ajali eneo la tukio  na kusababisha kifo cha dereva wake  Ndabashinze Paschal ( 46 )  aliyekuwa akitokea Dar Es Salaam kuelekea nchini Burundi.
Post Bottom Ad