Ajali/Picha-Malori yagongana, Yaua wawili Dar es Salaam. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Saturday, May 06, 2017

Ajali/Picha-Malori yagongana, Yaua wawili Dar es Salaam.

Watu wawili wamepoteza maisha na mmoja kujeruhiwa kwa kuvunjika mguu baada ya malori mawili kugongana eneo la Tabata Relini, Dar, usiku wa kuamkia leo May 6, 2017.

Imearifiwa kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa 9 usiku wa kuamkia leo baada ya lori aina ya Fuso kuligonga lori jingine kwa nyuma hivyo kusababisha ajali na maafa hayo.
Taarifa zaidi zimeeleza kuwa, kwenye fuso kulikuwa na watu watatu ambapo wawili walifariki dunia papo hapo na mmoja ambaye ni dereva alivunjika mguu hivyo baada ya kuokolewa alikimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.

Aidha Jeshi la Polisi na Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji wamewahi kufika eneo la tukio na kufanya uokozi.


Post Bottom Ad