Kamati Kuu
ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imewateua washiriki sita
kugombea Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Katika kikao
kilichofanyika jana,May 02,2017 mjini Zanzibar walioteuliwa ni Profesa Abdalla Safari,
Salum Mwalimu, Ezekiel Wenje, Josephine Lemoyan, Lawrence Masha na Pamela
Massay.
Taarifa ya
leo iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya CHADEMA, Bw.Tumaini
Makene imesema wateule hao watakamilisha hatua zingine za uteuzi kwa mujibu wa
utaratibu, Kanuni za Bunge na Uchaguzi wa Bunge la Afrika Mashariki.
Masha na
Wenje, walishiriki uchaguzi uliofanyika Aprili 4,2017 ambao CHADEMA ilipeleka majina
yao pekee jambo lililozua mjadala bungeni na kuhitimishwa kwa wao kupigiwa kura
za Hapana.
Katika
uchaguzi huo, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano waliwachagua Wajumbe Saba
wa EALA.
Kwa upande
wa CCM, walioshinda ni Fancy Nkuhi, Happiness Legiko, Maryam Ussi Yahya, Dk
Abdullah Makame, Dk Ngwaru Maghembe na Adam Kimbisa na kutoka CUF iliyokuwa na
wagombea watatu kwa ajili ya nafasi moja, aliyeshinda ni Mohamed Habib Mnyaa
akiwashinda Twaha Taslima na Sonia Magogo.
|
No comments:
Post a Comment