pesaaa

DSTV

Header Banner

EPL 2016/2017-Liverpool Yarejea Nafasi ya 3 ,Ikiishinda Watford 0 -1.

Mchezaji Emre Can akifanikiwa kuifungia Timu yake ya Liverpool bao pekee katika dakika ya 45  hapo Jana usiku Mei 01,2017,katika ushindi wa  bao 1-0 dhidi ya wenyeji, Watford kwenye Uwanja wa Vicarage Road kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England 2016/2017.

 

Ushindi huo unairudisha Liverpool nafasi ya tatu ikifikisha pointi 69 na kuishushia nafasi ya nne, Manchester City wenye Pointi 66,nafasi ya 5 ni Manchester United Pointi 65 na nafasi ya 6 wako Arsenal wakiwa na Pointi 60 za mechi 33.

Chelsea wanaongoza Ligi kwa Pointi 81 za mechi 34 wakifuatiwa na Tottenham Hotspur wenye Pointi 77 za mechi 34.