Meli kubwa
ya kubeba Ndege ya Marekani ya Carl Vinson ikiwa Kusini mwa Japan Jumamosi
April 29,2017.
|
Izumo ndiyo
meli kubwa zaidi ya kivita ya Japan.
Na ni ndiyo
ambayo ni fahari ya Jeshi la Wanamaji la Japan, na kufikia sasa ndiyo meli
kubwa zaidi ya Jeshi hilo.
Izumo ina
urefu wa mita 249 na inaweza kubeba helikopta hadi tisa.
Inafanana
sana na meli za kivita za kushambulia adui majini za Marekani ambazo
zinamilikiwa na Marekani, gazeti la Japan Times linasema.
|
Picha za
televisheni za Japan zilionesha meli ya Izumo ikiondoka bandari ya Yokosuka.
Taifa la Japan
limeituma meli yake kubwa zaidi ya kivita baharini, hatua yake ya kwanza ya
aina hiyo tangu kupitishwa kwa sheria mpya yenye utata iliyowezesha taifa hilo
kuanza kupanua uwezo wa Jeshi lake.
Meli hiyo
kubwa ya kubeba helikopta ambayo imepewa jina Izumo imetumwa kuifuata meli ya
kubeba mizigo na vifaa vya kijeshi ya Marekani ambayo inapitia katika maeneo ya
bahari ya Japan.
Meli hiyo ya
Marekani inaelekea kufikisha mafuta kwa meli nyingine za taifa hilo
zinalohudumu eneo hilo, ikiwemo meli yake kubwa ya kubeba ndege ya Carl Vinson
na meli zinazoandamana na meli hiyo karibu na rasi ya Korea.
Korea
Kaskazini imetishia kuizamisha Carl Vinson pamoja na nyambizi ya Marekani, huku
wasiwasi ukiendelea kuongezeka eneo hilo.
Shirika la
habari la Kyodo limesema meli hiyo imeondoka kwenye kambi yake eneo la Yokosuka
kusini mwa Tokyo kwenda kuungana na meli hiyo ya kusafirisha bidhaa za jeshi la
Marekani, na kwamba itaisindikiza hadi kwenye pwani ya Shikoku magharibi mwa
Japan.
|
No comments:
Post a Comment