Arsenal yapanda Nafasi ya 5 baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Southampton. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 11, 2017

Arsenal yapanda Nafasi ya 5 baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Southampton.

Timu ya Arsenal imeimarisha matumaini yao ya kutaka kuwa katika timu nne bora katika msimamo wa Ligi kuu ya Uingereza kufuatia ushindi wao wa mabao 2-0 dhidi ya Southampton.

Mabao hayo yalifungwa na Alexi Sanchez na Olivier Giroud huku Southampton hawakufanya mashambulizi mengi katika safu ya ulinzi ya Arsenal.Ushindi huo unamaanisha kwamba Arsenal imepanda juu ya Manchester United katika nafasi ya 5 ,alama tatu nyuma ya Manchester City.

Msimamo wa EPL.
Baada ya kipindi cha kwanza kilichokosa mchezo mzuri Sanchez Pichani aliwashangaza wengi baada ya kuwachenga walinzi wa Southampton na kisha kucheka na wavu.

EPL itaendelea kesho Ijumaa kwa Mechi mbili ambazo Everton itacheza na Watford na Vinara Chelsea kuwa Ugenini huko The Hawthorns wakihitaji kuifunga tu West Bromwich Albion ili kutwaa Ubingwa wakiwa na Mechi moja mkononi.

EPL - LIGI KUU ENGLAND 2016/2017.

Ijumaa Mei 12,2017.

2145 Everton v Watford             

2200 West Bromwich Albion v Chelsea            

Jumamosi Mei 13,2017.

1430 Manchester City v Leicester City            

1700 Bournemouth v Burnley               

1700 Middlesbrough v Southampton    

1700 Sunderland v Swansea City

1930 Stoke City v Arsenal

Jumapili Mei 14,2017.

1400 Crystal Palace v Hull City   

1615 West Ham United v Liverpool      

1830 Tottenham Hotspur v Manchester United

Post Bottom Ad