Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2016/2017 -Jijini Cardiff ni Juventus dhidi Real Madrid. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 11, 2017

Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2016/2017 -Jijini Cardiff ni Juventus dhidi Real Madrid.

Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya 2016/2017  Itachezwa Juni 3,2017 huko Jijini Cardiff na itawakutanisha Timu ya Juventus ya Italia dhidi ya mabingwa watetezi Real Madrid kutoka Hisopania.

Hapo jana May 10, 2017, Real Madrid imepoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Atletico Madrid.

Alianza Saul Niguez dakika ya 12 kuzichungulia nyavu za Real Madrid kabla ya Antoine Griezman dakika ya 16 kuiandikia Atletico bao la pili kwa mkwaju wa penati.

Lakini wakati Atletico wakiamini wangemaliza kipindi cha kwanza wakiongoza kwa goli 2 - 0, dakika ya 42, Isco alifanikiwa kuipatia Real Madrid goli na kuufanya mchezo huo kwenda mapumziko kwa bao 2 kwa 1.


Bao la Isco lilikuwa la kwanza kwake katika michezo yake 31 iliyopita katika Champions League, na bao hilo liliifanya Real Madrid kufunga mfululizo goli katika mechi 67 mfululizo.

Kipindi cha pili Atletico iliwapasa kufunga mabao mengine matatu ili kuitoa Real Madrid na walishindwa  kutafuta mabao hayo na mchezo kuisha kwa bao 2 – 1 na Real Madrid imefuzu kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya ushindi wa 3-0 kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.


Matokeo hayo yameifanya Real Madrid kufudhu kwenda katika fainali ya Champions League msimu huu na hii ikiwa ni mara mbili mfululizo katika misimu miwili.

Real Madrid sasa wanaifuata Juventus ambao usiku wa Jumanne waliitoa AS Monaco ya Ufaransa na sasa ni fainali ya vigogo na wakongwe kutoka Hispania na Italia.
Post Bottom Ad