Yanga SC sasa yahitaji sare dhidi ya MC Alger ili wafuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 08, 2017

Yanga SC sasa yahitaji sare dhidi ya MC Alger ili wafuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.

Goli  la kiungo Mzimbabwe, Thabani Scara Kamusoko limeipa Timu ya Yanga SC ushindi wa bao 1-0 dhidi ya MC Aalger katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la CAF la Shirikisho Afrika jioni ya leo,April 8, 2017 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 

Mchezaji huyo alifunga bao hilo dakika ya 61 ya mchezo akimalizia pasi ya kiungo mshambuliaji Mzambia, Obrey Chirwa baada ya kazi nzuri ya kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima aliyepasua na  mpira kutokea nyuma.

Yanga SC sasa itahitaji sare au ushindi katika mchezo wa marudiano wiki ijayo mjini Algiers dhidi ya Timu ya MC Alger ili wafuzu kwenda hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho kwa mara ya pili mfululizo mwaka huu.

Post Bottom Ad