Taswira Picha Manchester United wakiitwanga Chelsea Mechi ya EPL leo April 16,2017. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 16, 2017

Taswira Picha Manchester United wakiitwanga Chelsea Mechi ya EPL leo April 16,2017.

Wenyeji Manchester United wamewatandika Vinara wa Ligi Kuu England 2016/2017,  Chelsea bao 2-0 na kujiweka hai kumaliza 4 Bora huku wakiacha mbio za Ubingwa kuwa wazi.

Bao za Man United, hii Leo April 16,2017 zilifungwa na Marcus Rashford Dakika ya 7 kwa pande kali la Ander Herrera huku Dakika ya 49 shambulizi kali la Man United lilizua kizaazaa Golini mwa Chelsea na pasi ya Ashley Young kumfikia Ander Herrera alieachia kigongo kilichombabatiza Zouma na kutinga golini.
 


Ushindi huu wa Manchester United umewaweka Nafasi ya 5 wakiwa Pointi 4 nyuma ya Timu ya 4 Man City huku wao wakiwa na Mechi 1 mkononi.

Chelsea bado wanaongoza EPL lakini sasa tofauti ya Pointi na Timu ya Pili Tottenham ni Pointi 4 na Mechi zimebaki 6.


Kwenye Mechi iliyochezwa awali Leo huko The Hawthorns, Bao la Dakika ya 46 la Roberto Firmino  EPL-APR16limewapa Liverpool ushindi wa 1-0 dhidi ya West Bromwich Albion na kupaa hadi Nafasi ya 3.

Post Bottom Ad