Msimamo Ligi Kuu Vodacom Tanzania 2016/2017 ulivyo kwa sasa kwa timu 10 za Juu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, April 16, 2017

Msimamo Ligi Kuu Vodacom Tanzania 2016/2017 ulivyo kwa sasa kwa timu 10 za Juu.

Hapo jana April 15, 2017 -Simba SC ilikwama  baada ya kuambulia sare ya 0-0 mbele ya wenyeji Toto Africans Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza. 

Matokeo hayo yanaiongezea pointi moja Simba SC ikifikisha pointi 62 pamoja na zile tatu za mezani walizopewa kwa madai Mohammed Fakhi alicheza akiwa ana kadi tatu za njano baada ya kufungwa na Kagera Suagr 2-1.

Maana yake Simba SC inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.

Kwenye Mechi zingine za VPL - JKT Ruvu na Azam FC zilitoka 2-2, Stand United na Mtibwa Sugar 0-0 na Ruvu Shooting kuichapa Maji Maji FC 4-1.

VPL imeendelea leo Jumapili April 17,2017 kwa Mwadui FC kuikaribisha Ndanda FC na Mbao FC kuwa Wenyeji wa Tanzania Prisons.

Post Bottom Ad