Taswira Namna Juhudi za Messi na Neymar hazikufua dafu -Barcelona ikifa 3-0 Klabu Bingwa Ulaya. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, April 12, 2017

Taswira Namna Juhudi za Messi na Neymar hazikufua dafu -Barcelona ikifa 3-0 Klabu Bingwa Ulaya.

Juhudi za Messi na Neymar hazikufua dafu.

FC Barcelona walichapwa magoli 3-0 na Juventus katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2016/2017.

Paulo Dybala alifunga magoli mawili katika dakika ya 7 na ya 22. Bao la tatu lilifungwa na Giorgio Chiellini katika dakika ya 55.

Barcelona walicheza kufa na kupona kujaribu kupata japo bao moja la ugenini lakini hawakuweza kufua dafu.Barcelona's head coach Luis Enrique.
Wachezaji wa Juventus na furaha ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Barcelona.

Mechi nyingine iliyopaswa kuchezwa Jana kati ya Borussia Dortmund na Monaco iliahirishwa baada ya Basi ambalo liliwachukua Timu ya Dortmund kukumbwa na Milipuko na kumjeruhi Mchezaji wao mmoja Marc Bartra.

UEFA imeamua Mechi hii ichezwe Leo April 12, 2017 sambamba na Mechi nyingine mbili ambazo ni za huko Allianz Arena Jijini Munich kati ya Bayern Munich na Mabingwa Watetezi Real Madrid na nyingine ni huko Spain kati ya Atletico Madrid na Leicester City.

Post Bottom Ad