Taswira Picha Gari la Borussia Dortmund lililengwa na Milipuko Mitatu. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 12, 2017

Taswira Picha Gari la Borussia Dortmund lililengwa na Milipuko Mitatu.


Hapo Jana April 11, 2017, Usiku  Mchezo wa hatua ya robo fainali ya UEFA Champions League 2016/2017 kati ya Timu ya Borussia Dortmund dhidi ya Monaco uliahirishwa kwa sababu za kiusalama, baada ya Borussia Dortmund kushambuliwa saa chache wakiwa wanaelekea uwanjani kwa ajili ya mechi hiyo.

Tukio hilo la shambulio lilitokea Ujerumani kwa mujibu wa mtandao wa BBC News na kuwa shambulizi hilo linahusishwa na kikundi cha Islamist kutoka Syria na mchezaji Marc Bartra ndio mchezaji pekee wa Dortmund aliyeumia katika tukio hilo na amefanyiwa upasuaji.


Polisi nchini Ujerumani imesema kuwa licha ya gari hilo kuwabeba wachezaji wa Borussia Dortmund kuelekea katika mchezo wa nyumbani kwenye ligi ya mabingwa Ulaya lililengwa na milipuko mitatu na wamesema kuwa barua ilikutwa pembezoni mwa eneo la shambulizi hilo,lakini haikuwa na maelezo ya kutosha.

Polisi imekana kuwa ni shambulizi la kigaidi.

Mlinzi Marc Bartra amejeruhiwa katika shambulizi hilo

Taarifa za kiintelijensia zinasema kuwa zinachunguza shambulizi hilo kama linahusika na mashabiki wa timu ya upinzani.

Mchezo kati ya Borussia Dortmund v Monaco inachezwa leo (Itaanza Saa 1 Dakika 45 Usiku)

Marc Bartra alifanyiwa upasuaji wa mkono wake usiku huo huo wa April 11,2017 baada ya kuvunjika mfupa kutokana na tukio hilo, Marc Bartra mwenye umri wa miaka 26 amekuwa mchezaji muhimu wa Dortmund akiwa kaichezea timu hiyo katika michezo 30.Post Bottom Ad