Naibu Waziri
wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema kwamba,uhalifu wa aina yoyote utakao
fanya na mtu yoyote,wa chama chochote, dhidi ya raia yoyote ikiwemo waandishi
wa habari na Jeshi la Polisi, atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Naibu Masauni
ameyasema hayo Leo April 27,2017 mjini Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Kilombero, Peter
Lijualikali lililohoji, je”, Ni juzi tu hapa nimetoka kwenye
uchaguzi mdogo Ifakara tarehe 23 ambapo kwanza Mwandishi wa Mwananchi, Juma
Mtanda alitekwa na wanachama na wafuasi wa CCM wakampora Ipad, wakampora simu,
wakampora na kamera, matokeo yake Polisi wakawatafuta watu wa CCM na
wakamrudishia vifaa vyake.
... maana yake Polisi wanawajua waliofanya uhalifu huu,
lakini mpaka leo hakuna kilichofanyika, hakuna kesi hakuna chochote, lakini
kwenye uchaguzi ule askari alipigwa na tofali kapasuka ameshonwa nyuzi tano na
amepigwa na wanachama wa CCM lakini Polisi wana muachia anatembea anafanya
chochote, sasa naomba waziri aniambie kama CCM wanaruhusiwa kufanya vurugu
kutaka kujeruhi askari wetu alafu wakaachiwa huru, naomba nijibiwe.
Akijibj
swali hilo, Mheshimiwa Masauni alisema, “Mheshimiwa Lijualikali anazungumzia
tuhuma za CCM kuwajeruhi askari Polisi lakini pia kupora waandishi wa habari,
Mheshimiwa Naibu spika kwanza kabisa nashindwa kulijibu suala hili moja kwa
moja, kwasababu unapozungumzia tuhuma ni kwamba hawa ni wafuasi wa chama fulani
inahitaji uthibitisho, ninachoweza kusema uhalifu wa aina yoyote utakao fanya
na mtu yoyote wa chama chochote dhidi ya raia yoyote ikiwemo waandishi wa
habari na Jeshi la Polisi ndiyo kabisa maana jeshi la Polisi lipo hapa kwaajili
ya kulinda usalama wetu hatutakubali kamwe.”
“Mtu yoyote
asicheze na Jeshi la Polisi na sio tu jeshi la Polisi hata waandishi wa habari,
wamekuwa wakifanya kazi nzuri sana ya kuweza kuhabarisha jamii na kutoa taarifa
nzuri kwa umma. Hivyo hatuwezi kukubali waandishi wa habari au Jeshi la polisi
kuweza kufanyia matukio yoyote ya kihalifu na raia mwingine yoyote tutachukua
hatua kali za kisheria, kwahiyo muheshimiwa mbunge kama una ushahidi wa hilo
jambo ulete kwahiyo siwezi sema chama fulani kimefanya jambo fulani bila
uthibitisho.”
|
No comments:
Post a Comment