Picha kuhusu Operesheni Ondoa Mifugoa Kagera Sehemu ya Pili. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, April 08, 2017

Picha kuhusu Operesheni Ondoa Mifugoa Kagera Sehemu ya Pili.

Na: Sylvester Raphael.

Operesheni ondoa mifugo katika Hifadhi za Misitu na Mapori ya Akiba Mkoani Kagera yaendelea kwa kasi ambapo tangu kuanza kwa operesheni hiyo Machi 31, 2017 hadi kufikia Aprili 7, 2107 tayari  mifugo 4489 imekamatwa na watuhumiwa wa makosa mbalimbali 115 wametiwa mbaloni.

Mifugo iliyokamatwa ni pamoja na Ng’ombe 4328, Mbuzi 125 na Kondoo 36. Pia watuhumiwa 115 waliokamatwa kwa makosa mbalimbali  Watanzania ni 109, Warundi 4 na Wanyarwanda 2. 

Aidha Ng’ombe 144, kondoo 17 na mbuzi 113 wametaifishwa na Serikali baada ya watuhumiwa kushindwa kesi zao na Mahakamani kuiamurisha Serikali kutaifisha mifugo hiyo.

Serikali ya Mkoa wa Kagera katika kuhakikisha zoezi la operesheni linafanikiwa kwa asilimia 100%  imeanza  kutumika ndege zisizotumia Rubani (Drones) pia na ndege zinazotumia Rubani ili kukagua maeneo yote ambayo siyo rahisi kuonwa au kufikika na vikosi vya nchi kavu ambako mifugo hufichwa na wavamizi na kuendesha shuguli za kinadamu.


Akirusha ndege isiyotumia Rubani katika kituo Kiteule cha Nyakanazi  Bw. Parmena Pallangyo Afisa Wanyamapori kutoka Pori la Akiba la Lwikwika Lumesule lililopo Wilayani Masasi Mkoani Mtwara alisema ndege hizo zina uwezo wa kusafiri zaidi ya Kilometa 10 kwa muda mfupi zikiwa zinapiga picha mnato na picha za video kwa kuonesha viwianishi (coordinates) za kila eneo kila kitu kilichopo ardhini.

Badala ya kuangaingaka na kutumia rasilimali magari, mafuta au rasilimali watu kwenda kutafuta mifugo katika maeneo ambayo hatuna uhakika, tunazituma kwanza ndege hizi zinatuletea taarifa za picha na eneo walipo mifugo pia picha hizo zinakuwa na viwianishi (coordinates) ambazo zinatusaidia kujua eneo husika ndipo sasa vikosi vinaelekezwa eneo husika na kwa kutumia kifaa kiitwacho GPS huwawezesha  kukamata mifugo hiyo.” Alifafanua Bw. Parmena 



Wafugaji na Wafanyabiashara wa Ng’ombe wasemaje?

Katika Mnada wa Ng’ombe wa Rusahunga ambao hufanyika kila siku ya Alhamisi kila wiki wanunuzi wa Ng’ombe wanasema kuwa kwasasa Ng’ombe wanapatikana kwa wingi katika Mnada. 

Bw. Sena Elias Magoma mnunuzi  alisema kuwa kwa Ng’ombe aliyekuwa anauzwa bei ya shilingi 1,200,000/=  wiki mbili zilizopita kwasasa anauzwa bei ya shilingi 800,000/= hadi 700,000/= na aliyekuwa anauzwa shilingi 500,000/= kwasasa anauzwa shilingi 300,000/= hadi 250,000/=.

Naye Bw. Fikiri Matenya Mashine  ambaye ni mfugaji alisema kuwa katika mnada huo kwa sasa Ng’ombe ni wengi kiasi kwamba bei imeshuka sana na wafugaji wanawarudisha ng’ombe wao nyumbani kwakukosa soko. 

Akiulizwa sababu ya ngo’ombe kuwa wengi katika mnada huo wa Rusahunga kwasasa na bei kushuka alisema;

“Mimi nadhani kutokana naparancha’  (akimaanisha operesheni) linaloendelea huko maporini ndiyo maana ng’ ombe wamekuwa wengi katika mnada na pengine matajiri wanasubiri mnada wa ng’ombe ambao Serikali imewakamata ili wawanunue kwenye mnada kwa bei ya chini sana. 

Lakini mimi naona Serikali imefanya jambo jema hawa Wafugaji kutoka nje ya nchi wanatunyanyasa sana kama watondoka mimi naamini kuwa malisho yatatutosha sisi wenyeji.” Alifafanua Bw. Mashine

Aidha, Afisa Mifugo anayesimamia Mnada wa Rusahunga Bw. Raphael Barakekenwa alisema kwa kipindi hiki cha operesheni mifugo hasa ng’ombe wamekuwa wengi mno kiasi kwamba wanakosa soko lakini Serikali kuu na Halmashauri zinapata mapato ya kutosha kutokana na wingi wa ng’ombe mnadani.

 Pia alitoa angalizo kuwa kwa wiki mbili au tatu zijazo huenda kukawa na uhaba mkubwa wa nyama sokoni kwasababu ng’ombe wengi kuondolewa maporini na kusafishwa kwenda mikoani na nje ya nchi.

Vilevile katika mnada huo Mwandishi wa habari hii alishuhudia malori mengi yakiwa yanapakia ng’ombe kwa wingi na kuondoka kuelekea mikoani pia ng’ombe wengi wakiwa katika eneo hilo la mnada wa Rusahunga wakisubiri kununuliwa aidha wafugaji wengine wakiamua kurudi nyumbani na ng’ombe wao waliokosa soko katika mnada huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad