Msichana
mmoja (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa mika 16 na mwanafunzi wa kidato cha 3
huko Zanzibar, juzi alijitosa baharini katika eneo la Chumbe kutoka katika boti
ya Azam Marine Kilimanjaro V.
Msichana
huyo aliyekuwa akisafiri na mjomba wake kutoka Dar es salaam kwenda Unguja
alijirusha baharini majira ya saa 5 na kuokolewa na mabaharia wa boti hiyo
ndani ya muda mchache.
Wanafamilia
wa binti huyo waishio eneo la Kikwajuni Unguja walieleza kuwa kabla ya kutoroka
kwa binti huyo, walimkuta na simu ambayo hawakufahamu alikoipata.
Kutokana na
utaratibu wa familia hiyo ya kutoruhusu simu kwa watoto, walimnyang’anya simu
hiyo na kumtaka aeleze alikoitoa vinginevyo watampeleka Polisi. Binti huyo
alikasirishwa na kitendo hicho ndipo alipofanya uamuzi wa kutoroka.
Mama mdogo
wa binti huyo alieleza kuwa walimtafuta binti huyo bila mafanikio ndipo
walipoamua kuipekua simu aliyokuwa akiitumia na kukuta namba ya kijana mmoja
iliyokuwa imetumiwa mara nyingi.
Walipowasiliana na kijana huyo kumuuliza
anafahamiana vipi na yule binti, alijibu kuwa walijuana kupitia mtandao wa
‘facebook’ lakini hawajawahi kukutana kwa kuwa binti anaishi Zanzibar na kijana
anaishi Dar es Salaam.
Alisema
walimpa taarifa kijana huuyo kuwa binti yao ametoroka na hajulikani
alikokwenda, hivyo kumwomba kusaidiana kuhakikisha wanampata akiwa salama.
“Kwa kweli
kijana huyo alikubali kutoa ushirikiano na akawa anawasiliana na binti yetu na
kumuleza kuwa yuko Dar es Salaam na amehifadhiwa na dereva teksi baada ya
kukosa msaada wa eneo analotaka kwenda ambako ni kwa bibi yake anayeishi
Mburahati, Dar es Salaam” alisema
Alisema
aliwasiliana na dereva huyo aliyemuhifadhi binti yao na kuambiwa kwamba
amesharipoti katika serikali ya mtaa anoishi kuwa amemuokota binti huyo
bandarini , Dar es salaam baada ya kukaa kwa muda mrefu bila ya kupata msaada.
Mama mdogo
ambaye ndiye aliyemlea binti huyo tangu akiwa mdogo alieleza kwamba mama mzazi
wa binti huyo anaishi Muscat, Oman, na
alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kupata taarifa kuwa binti yake amejitupa
baharini wakati akitokea Dar es Salaam baada ya kusakwa kwa siku kadhaa na
hatimaye kupatikana.
Naye mjomba
wa binti huyo ambaye ndiye aliyekwenda Dar es Salaam kumchukua, alieleza kuwa
wakiwa ndani ya boti binti alilalamika kuwa anajisikia vibaya, hivyo anahitaji
kwenda kukaa kwenye veranda ya boti ili apunge upepo. Wakatoka kwenda kwenye
veranda nje ya boti hiyo.
Wakiwa
wamekaa binti huyo alimtaka mjomba wake kumpatia kitambaa cha kufunika uso
‘nikabu’ na baibui avae ili kuepuka usumbufu wakati wa kushuka kwani muda wa
kufika Zanzibar ulikuwa umekaribia.
Mjomba
alipogeuka upande wa pili ili kuvichukua vitu hivyo katika begi, ndipo ghafla msichana huyo
alijitosa ndani ya bahari.
“Nilipiga
yowe baada ya kuangalia na kumwona. Tulishirikiana na mabaharia wa boti
hiyo ili kumwokoa na ndani ya muda
mchahe tulifanikiwa” alisema
Wanafamilia
wa binti huyo walisema binti huyo alikuwa na tabia nzuri tokea alipokuwa mdogo,
na mara nyingi alipendelea kukaa ndani. “Hatujui kwa nini amliamua kufanya
uamuzi huo”
Aidha
daktari Suleiman Abdul, Mratibu wa huduma za afya Hospitali ya Kidongo Chekundu
alikotibiwa msichana huyo, alisema wanaendelea na uchunguzi wa afya ya akili ya
msichana huyo na kuwataka wanafamilia yake kutokuzungumzia chochote kuhusu
tukio hilo na waendelee kushirikiana nae vizuri ili kuona maendeleo ya afya
yake.
|
No comments:
Post a Comment