Makamo
Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri wa Habari (TEF), Deudatus Balile (kulia) ,
akipokea mfano wa hundi wa shilingi milioni 14 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji
kiwanda cha Saruji cha Tanga Simba
Cement, Renhardt Swart, kusaidia jukwaa hilo katika majukumu yake ya kila siku
ikiwemo mkutano wao mkuu kesho Moshi Mkoani Kilimanjaro.
|
Afisa
Mawasiliano na Masoko kiwanda cha Saruji cha Simba Cement Tanga , Hellen
Maleko, (kulia) akiwakabidhi hundi yenye mfano wa shilingi milioni 14 Wahariri
wa Jukwaa la vyombo vya habari mara baada ya kutembelea kiwanda hicho leo ikiwa
ni msaada katika mambo yao mbalimbali ukiwemo mkutano wao mkuu kesho Moshi
Mkoani Kilimanjaro.
|
Kiwanda Cha
Saruji cha Simba Cement Tanga, kimesema moja ya faida yake imekuwa ikiipeleka
katika masuala ya kijamii yakiwemo, Afya, Mazingira na Elimu.
Akizungumza
mara baada ya Wahariri (Jukwaa la Wahariri TEF)
kumaliza ziara ya kutembelea
kiwanda cha Saruji kujionea shughuli ambazo zinafanywa, Mkurugenzi Mtendaji wa
kiwanda hicho, Renhardt Swart, alisema moja ya faida huipeleka kwa wananchi.
Alisema
wamekuwa wakisaidia madawati, mifuko ya saruji na majengo pamoja na vyoo kwa
shule ambazo zimekuwa zikihitaji msaada.
Akikabidhi
shilingi milioni 14 kwa Jukwaa hilo, Swart alisema pesa hizo zinaweza
kuwasaidia katika majukumu yao
mbalimbali ukiwemo mkutano mkuu ambao utafanyika kesho Moshi Mkoani
Kilimanjaro.
Kwa upande
wake, Makamo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Deudas Balile, alisema
amefurahishwa na uzalishaji wa Saruji pamoja na mipango kabambe kiwandani hapo.
Akizungumzia
msaada huo, Balile alisema utasaidia katika masuala mbalimbali ya Jukwaa hilo
ikiwa na pamoja na mkutano mkuu wa Moshi
kesho na kutoa shukurani na kuwataka wawekezaji wengine kuiga mfano kama huo.
|
Wahariri
kutoka vyombo mbalimbali wakiangalia eneo uchumbani wa Matirial Kware kilometa
2 kutoka ndani ya eneo la kiwanda.
|
No comments:
Post a Comment