Wabunge watakaoiwakilisha Tanzania Bunge la Afrika Mashariki Wamepatikana. - Mwana Wa Makonda

Breaking

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 05, 2017

Wabunge watakaoiwakilisha Tanzania Bunge la Afrika Mashariki Wamepatikana.


Jana Jumanne,April 4, 2017 - Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipiga kura kuchagua wabunge watakaoiwakilisha nchi katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kwa kipindi cha miaka mitano.

Baada ya mvutano wa muda mrefu kuhusu uchaguzi huo, ulifanyika na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutangaza orodha ya washindi waliochaguliwa kuiwakilisha nchi.

 Tanzania inatakiwa kutoa wabunge 9 kwenda EALA, lakini matokeo ya jana yalitangaza washindi saba tu baada ya wagombea wawili kupigiwa kura nyingi za hapana, na hivyo kuonekana kuwa wabunge hawakuwataka.

Kati ya wabunge 7 waliotangazwa, 6 ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na mmoja na wa Chama cha Wananchi (CUF).

Wagombea wa CHADEMA, Lawrence Masha na Ezekiah Wenje walipingwa kwa kupigiwa kura nyingi za hapana.

Post Bottom Ad