Katika ziara
hiyo Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia makontena 20 ya mchanga wenye madini kutoka
kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa ambayo yamezuiliwa kusafirishwa nje ya nchi
tangu alipotoa agizo la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya nchi
tarehe 02 Machi, 2017.
Pamoja na
kushuhudia makontena hayo, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la
Polisi Nchini IGP – Ernest Mangu na vyombo vingine vya dola kuhakikisha mchanga
wa madini unashikiliwa popote ulipo, mpaka hapo uchunguzi wa kina
utakapofanyika kubaini ukweli.
“Nataka
niwaambie nchi yetu inachezewa mno, nimekuja kuyaona haya makontena kama yapo,
na kweli nimeyaona, sasa utaratibu utakapokamilika nataka Watanzania na dunia
nzima ione kilichomo humu ndani kama ni mchanga kweli ama dhahabu” amesema Mhe.
Rais Magufuli.
|
Rais
Magufuli akifamnya ukaguzi bandarini hapo.
Akiwa
bandarini hapo Mhe. Dkt. Magufuli pia ameshuhudia udanganyifu mwingine
unaofanywa na wafanyabiashara wanaoagiza mizigo kutoka nje ya nchi baada ya
kuoneshwa makontena ambayo nyaraka zinaonesha yamebeba mitumba ya nguo na viatu
wakati ndani yake kila kontena moja limebeba magari matatu ya kifahari.
Maafisa wa
bandari ya Dar es Salaam na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamemueleza Mhe.
Rais Magufuli kuwa kufuatia maelekezo aliyoyatoa ya kuhakikisha mizigo yote
inakaguliwa kwa mitambo ya mionzi (Scanning Machines) wamefanikiwa kubaini
udanganyifu mwingi unaofanywa na wafanyabiashara wanaoingiza nchini na
kusafirisha nje ya nchi mizigo mbalimbali yakiwemo makontena 10 ambayo
yamepatikana yakiwa na magari ya kifahari ilihali nyaraka zake zikionesha yana
mitumba ya nguo na viatu.
|
Mhe. Rais
Magufuli amewapongeza maafisa na wafanyakazi wa bandari ya Dar es Salaam na TRA
kwa kazi nzuri wanayofanya kudhibiti upotevu wa fedha za umma bandarini hapo na
amewataka kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa uzalendo na kujiepusha na rushwa.
“Leo mmenifurahisha
sana, ninawatia moyo endeleeni kuwakamata wote wanaofanya udanganyifu huu na
muwachukulie hatua kali za kisheria, lakini msimuonee mtu na msipokee rushwa,
tunataka watu wajifunze kuwa hapa sio shamba la bibi” amesisitiza Rais
Magufuli.
Aidha,
ametoa wito kwa vyombo vyote vinavyoshughulikia udhibiti wa mizigo inayoingia
na kutoka kupitia bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine hapa nchini,
kuendelea kushirikiana ili kukomesha vitendo vyote vya udanganyifu ambavyo
vinasababisha nchi kupoteza mapato mengi.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam
23 Machi,
2017
|
No comments:
Post a Comment