Baada ya taarifa ya IKULU:Hiki ndicho Kimeandikwa na Nape Nnauye,Zitto Kabwe na TFF. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 23, 2017

Baada ya taarifa ya IKULU:Hiki ndicho Kimeandikwa na Nape Nnauye,Zitto Kabwe na TFF.

Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amewaomba wananchi watulie kufuiatia kutenguiliwa kwake kwenye nafasi hiyo ambayo imechukuliwa na aliyekuwa Waziri wa Sheria na Katiba, Dkt. Harrison Mwakyembe.

..'' Ndugu zangu naomba TUTULIE! LEO mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba TUTULIE..!

Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limempongeza Dkt Mwakwembe kufuatia uteuzi wake.

Kiongozi wa chama cha Alliance for Change & Transparency –ACT Wazalendo nchini Tanzania Mhe.Zitto Kabwe amesema Waziri wa habari aliyefutwa kazi Bw Nape Nnauye "ni shujaa".

Kwenye Twitter, Mhe. Kabwe, ambaye ni Mbunge wa Kigoma-Ujiji ,amesema amewasiliana na Bw Nnauye ambaye amemthibitishia kwamba ni kweli ameondolewa kwenye wadhifa wake wa uwaziri.
Taarifa kutoka ikulu mapema leo,March 23, 2017 ilitangaza Waziri mpya wa habari, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Dkt. Harrison George Mwakyembe.

Taarifa hiyo haikusema chochote kuhusu hatima ya Mhe.Nnauye.

Dkt Mwakyembe alikuwa  akihudumu kama Waziri wa Katiba na Sheria.

Mhe. Nnauye kwenye Twitter amewaomba watu kuwa na subira na kuahidi kwamba atazungumza na wanahabari baadaye leo.
Hapa Chini Soma Taarifa ya Ikulu.

Post Bottom Ad