Nape Nnauye Atishiwa Bastola kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Thursday, March 23, 2017

Nape Nnauye Atishiwa Bastola kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari.

Aliyekuwa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye Alhamis hii ya March 23,2017 alilazimika kuzungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam akiwa amesimama juu ya gari nje ya ukumbi wa Protea Hotel baada ya polisi kutaka kuuzuia mkutano huo usifanyike.

Akiwa amezungukwa na kundi kubwa la waandishi wa habari, Nape alilaani kitendo cha askari kumnyooshea bunduki wakati alipokuwa akijiandaa kuzungumza na waandishi wa habari.

Post Bottom Ad