Taswira Picha Wadau wa familia ya soka wilayani Ngara wamejitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa mchezaji wa Benaco FC-Nuru Athuman aliyefariki kwa ajali ya gari. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, March 07, 2017

Taswira Picha Wadau wa familia ya soka wilayani Ngara wamejitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa mchezaji wa Benaco FC-Nuru Athuman aliyefariki kwa ajali ya gari.

Nahodha wa Timu ya Benaco FC-Mpoto Mohamed ama Mpotompoto ( jaket la blue ) akipanda Ndege katika uwanja wa Ndege wa Ngara/Ruganzo, jana March 06,2017, wilayani Ngara,mkoani Kagera tayari kwa safari ya kuelekea Hospitali ya KCMC-Moshi kutibiwa baada ya kupata Ajali iliyotokea eneo la Nyamahwa ,March 05,2017 baada ya gari walilokua wakisafiria aina ya Toyota Carrina  yenye namba za usajili T 619 CFP kupasuka tairi la mbele kushoto na kupinduka.

Katika picha kushoto ni Kaimu katibu mkuu wa chama cha soka wilaya ya Ngara-NDFA-Jofuramu Mohamed na Mpoto Mohamed maarufu Mpotompoto ambaye ni nahodha wa Benaco FC walijeruhiwa ambapo pamoja na kuruhusiwa kutoka hospitalini,Mpoto Mohamed amepewa rufaa ya kwenda hospitali ya KCMC Moshi kwa matibabu Zaidi baada ya kubainika kuumia vibaya sehemu za kifuani na mbavuni.

Wadau wa familia ya soka wilayani ngara mkoani Kagera,leo wamejitokeza kuuaga mwili wa aliyekuwa mchezaji wa Benaco FC-Nuru Athuman aliyefariki jana kwa ajali ya gari wakati timu yake ya Benaco FC ikienda kucheza mchezo wa kirafiki na Timu ya Rulenge Stars –mjini Rulenge.

Nuru Athuman amefia katika hospitali ya Nyamiaga wakati Madaktari wakijaribu kuokoa maisha yake kutokana na kuumia sehemu kubwa ya kichwa chake na mwili wake umesafirishwa kwa ndege kwenda kwao Babati Mkoani Manyara kwa ajili ya mazishi.

Ajali hiyo iliyotokea eneo la Nyamahwa ,March 05,2017 baada ya gari walilokua wakisafiria aina ya Toyota Carrina  yenye namba za usajili T 619 CFP kupasuka tairi la mbele kushoto na kupinduka.

Katika ajali hiyo Kaimu katibu mkuu wa chama cha soka wilaya ya Ngara-NDFA-Jofuramu Mohamed,Juma Rasi,Sospita Rasi na Mpoto Mohamed maarufu Mpotompoto ambaye ni nahodha wa Benaco FC walijeruhiwa ambapo pamoja na kuruhusiwa kutoka hospitalini,Mpoto Mohamed amepewa rufaa ya kwenda hospitali ya KCMC Moshi kwa matibabu Zaidi baada ya kubainika kuumia vibaya sehemu za kifuani na mbavuni.

Post Bottom Ad