VPL 2016/2017:Simba SC waomba ubingwa Azam FC. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Monday, March 06, 2017

VPL 2016/2017:Simba SC waomba ubingwa Azam FC.

Mshambuliaji wa Simba SC, Laudit Mavugo.

Benchi la ufundi la Simba SC chini ya kocha wake mkuu, Joseph Omog, raia wa Cameroon, limeweka wazi kwamba sasa wanaelekeza maombi yao yote kwa timu ya Azam FC kuweza kuwafunga wapinzani wao Yanga SC ili wawasafishie njia ya wao kutwaa Ubingwa msimu huu 2016/2017.

Simba SC itakuwa na faida ya matokeo ya mchezo huo kati ya Yanga SC na Azam FC ambao ulipangwa kuchezwa wikiendi hii lakini utapangiwa tarehe nyingine kutokana na timu zote mbili kuwa na majukumu ya kimataifa. 

Katika mchezo wa awali msimu huu, timu hizo hazikufungana.

Msimamo wa Ligi ulivyo baada ya Mechi ya Yanga SC v Mtibwa Sugar kutoka sare ya 0-0.

Kocha Msaidizi wa Simba SC, Jackson Mayanja, alisema wanaamini kwamba Azam FC watakuwa kizuizi kizuri kwa Yanga SC kuchukua pointi kwao ambapo kama wakifungwa mchezo huo, itakuwa faida kwao.

“Tunategemea kwamba Yanga SC watakwama watakapokutana na Azam FC kwa kupata matokeo mabaya ambayo kwetu itakuwa faida kwa sababu njia ya ubingwa itazidi kusafishika na hilo litakuwa jambo zuri kwetu. 

“Japo hatufikirii sana matokeo ya wapinzani wetu kwa sababu tunacheza mechi zetu na lengo ni kushinda na siyo jambo lingine na tunaamini kama tutafanya vizuri kwenye mechi hizo, basi kila kitu kitakuwa kizuri kwetu,” alisema Mayanja.

Post Bottom Ad