Real Madrid yashinda 3-1 mjini Napoli na kwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 6-2. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, March 08, 2017

Real Madrid yashinda 3-1 mjini Napoli na kwenda Robo Fainali kwa ushindi wa jumla wa 6-2.

Hapo Jana March 7, 2017 -Mabingwa Watetezi Real MadridM wakicheza Ugenini huko Stadio San Paolo Mjini Napoli Nchini Italia, walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Napoli magoli 3-1 katika Mechi ya Pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Klabu Bingwa barani Ulaya  na hivyo kutinga hatua ya Robo Fainali kwa Jumla ya Bao 6-2 kwa Mechi 2.

 Dakika ya 24 Napoli walienda 1-0 mbele kwa Bao la Dries Mertens.

Dakika ya 52 Kona ya Toni Kroos ilifungwa kwa Kichwa na Sergio Ramos huku Dakika ya 57 Kona nyingine ya Kroos ilimaliziwa na Ramos na Real Madrid kuandika Bao la Pili.

Real Madrid walipiga Bao lao la 3 Dakika ya 90 baada ya Shuti la Cristiano Ronaldo kuokolewa na Kipa Reina na Alvaro Morata, alietokea Benchi, kuukwamisha Mpira huo uliotemwa.

Hadi mwisho Napoli 1 Real 3.

Mechi za Pili

**Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku Saa za Bongo

**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza

Jumatano 8 Machi 2017

Barcelona v Paris Saint Germain [0-4]  
             
Borussia Dortmund v Benfica [0-1]  

Jumanne 14 Machi 2017

Juventus v FC Porto      [2-0] 

Leicester City v Sevilla [1-2]   
        
Jumatano 15 Machi 2017

Atl├ętico Madrid v Bayer 04 Leverkusen [4-2]  
            
Monaco v Manchester City [3-5]   

Post Bottom Ad