Bayern Munich wasonga Robo Fainali kwa Jumla ya Bao 10-2 dhidi ya Arsenal. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, March 08, 2017

Bayern Munich wasonga Robo Fainali kwa Jumla ya Bao 10-2 dhidi ya Arsenal.

Mashabiki zaidi ya 200 wa Arsenal wakiandamana usiku wa jana March 7, 2017 nje ya Uwanja wa Emirates kushinikiza kocha Arsene Wenger aondoke huku wameshika bango la kushinikiza asiongezewe mkataba mpya, baada ya kipigo cha mabao 5-1 dhidi ya Bayen Munich.
Timu ya Arsenal imeondoshwa katika hatua ya 16 bora ya Mashindano ya Klabu Bingwa ulaya msimu huu 2016/2017 wakiwa kwao Emirates Jijini London baada ya kucheza Mechi ya Pili huku wakihitajika kupindua kipigo cha 5-1 cha Mechi ya Kwanza ili kutinga hatua ya Robo Fainali na Wakajikuta wakitwangwa tena Bao 5-1 na Bayern Munich ya Ujerumani.
Hivyo Bayern Munich wanasonga Robo Fainali kwa Jumla ya Bao 10-2 kwa Mechi mbili.

Huu ni Msimu wa 7 mfululizo kwa Arsenal kushindwa kuvuka Hatua hii ya makundi.

Arsenal walianza Mechi hii kwa Dakika ya 19, Theo Walcott akawapa Arsenal Bao kwa Shuti kali lililomshinda Kipa Neuer.
Dakika ya 52 Sentahafu wa Arsenal Koscielny alimwangusha Lewandowski na Refa kutoa Penati na pia kumpa Kadi Nyekundu.

Penati hiyo ilifungwa na Lewandowski na kisha  Mvua ya Magoli ya Bayern ikashuka kwa kupiga Bao nyingine 4 Dakika za 68, 78, 80 na 85 kupitia Arjen Robben, Douglas Costa na Arturo Vidal, Bao 2.


Post Bottom Ad