Siku ya Wanaweke Duinian,Wanawake mjini Ngara walishiriki Usafi na Kutoa Msaada katika hospital ya Nyamiaga. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, March 08, 2017

Siku ya Wanaweke Duinian,Wanawake mjini Ngara walishiriki Usafi na Kutoa Msaada katika hospital ya Nyamiaga.

Picha ya Pamoja.

Wadau wa Maendelo kwa kushirikiana na Serikali wametakiwa kujitoa na kusaidia kuboresha mazingira ya afya ya mama na mtoto na kupunguza msongamano uliopo katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Nyamiaga wilayani Ngara mkoani Kagera.

Wito huo umetolewa na mganga mfawidhi Hospitali ya Nyamiaga Dr.Raphael Rwezaula wakati akitoa shukrani kwa Wadau walioungana na baadhi ya Wanawake waliofika hospitalini hapo,Leo hii March 8, 2017 kuwafariji wanawake waliolazwa hospitalin hapo ikiwa ni kusheherekea siku ya wanawake duniani.

Kuadhimisha Siku ya Wanaweke Duinian,Wanawake mjini Ngara walishiriki katika hospital ya Nyamiaga tumetembelea wazazi na watoto ,kugawa Msaada wa Vitu mbalimbali sambamba na Kufanya usafi wwa mazingira.

Kwa upande wake Afisa Muuguzi wa Hospitali hiyo Dr Hillary Nkonyagi amesema pamoja na wahudumu kuendelea kuhudumia kwa kujitoa bado kuna uhitaji mkubwa wa wauguzi ambao kama wangepatikana wangesaidia katika utoaji wa huduma bora za mama na mtoto.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya ya Ngara Bi Mwajuma Ngwamuo amesema kuwa ni wakati mwafaka kwa wanawake kupaza sauti zao kutokana na hali mbaya iliyopo katika wodi ya wazazi inayosababisha wazazi kulala watatu kitanda kimoja.

Post Bottom Ad