Rais Dkt. Magufuli atoa miezi minne Mradi wa maji wa NG’APA Mkoani Lindi Ukamilike. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 03, 2017

Rais Dkt. Magufuli atoa miezi minne Mradi wa maji wa NG’APA Mkoani Lindi Ukamilike.

Sehemu ya Mradi wa Maji wa Ng’apa mkoani Lindi ambao Rais Dkt. Magufuli ametoa miezi minne kwa mkandarasi anayejenga mradi huo ili uweze kukamilika haraka.

PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa Mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo mkoani Lindi unakamilika ndani ya miezi mine na si vinginevyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge mteule Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika karibu na mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo Mkoani Lindi.
Akiendelea na ziara yake mkoani Lindi, Rais Dkt Magufuli leo,March 03,2017 amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani humo na kutoa maagizo ili kuhakikisha wananchi wananufaika na jitihada za serikali za kuboresha maisha yao.

Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Lindi,  Godfrey Zambi kumnyang’anya pasi ya kusafiria (passport) Mkandarasi anayeshughulikia Mradi wa Maji wa Ngapa hadi hapo atakapokamilisha mradi huo.

Rais Magufuli ametoa maagizo hayo alipokwenda kukagua mradi huo wa maji ambao hadi sasa umetumia miaka 6 kujengwa lakini bado haijakamilika. 

Pamoja na kuagiza pasi ya mkandarasi ichukuliwe, Rais Magufuli amempa miezi miwili mkandarasi huyo kuhakikisha mradi unakamili huku RC Zambi akiwa na jukumu la kuhakikisha kuwa mkandarasi hatoki eneo hilo la mradi.

Mradi huo unaotarajiwa kumaliza tatizo la maji mkoani Lindi umegharimu TZS bilioni 29 ambapo hadi sasa mkandarasi amelipwa bilioni 21. 

Rais Magufuli amesema kuwa kama tatizo ni fedha ndio sababu mradi haumaliziki aambiwe ili atoe fedha serikali kuu kukamilisha wananchi waweze kupata maji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ng’apa mara baada ya kutembelea mradi wa Maji wa eneo hilo ambao unasuasua kukamilika. Rais Dkt. Magufuli ametoa miezi minne kwa Mkandarasi kampuni ya Overseas Infrastructure Alliance Private Limited ya India kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa mradi huo na sio kuleta visingizio.

Mradi huo wa maji ukikamilika unatarajiwa kuzaliwa maji zaidi ya lita milioni 6 kwa siku.

Rais Magufuli anatarajiwa kukamilisha ziara yake mkoani Lindi leo jioni ambapo ataanza safari ya kwenda mkoani Mtwara atapofanya ziara yake Jumamosi na Jumapili. Katika kuhitimisha ziara yake ya siku nne katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara, Rais Magufuli atahutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad