Godbless Lema Aachiwa kwa Dhamana. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Friday, March 03, 2017

Godbless Lema Aachiwa kwa Dhamana.

Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo Machi 3, 2017 imemuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha Mjini,  Godbless Lema, (CHADEMA).

Katika kesi hiyo iliyotolewa maamuzi majira ya saa 7:30 mchana, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Mjini baada ya kupitia hoja za mawakili pande zote imemwachia kwa dhamana hiyo kwa masharti ya wadhamini wawili na kusaini bondi ya shilingi milioni tatu.

Lema amekaa mahabusu kwa takribani miezi minne sasa tangu alipokamatwa mwezi Novemba,2016 mjini Dodoma na kusafirishwa kupelekwa Arusha kisha kufunguliwa kesi ya uchochezi.

Post Bottom Ad