Radi kutoka
mawinguni kwenda ardhini inaweza kuleta hasara na madhara kwa watu au vitu,
watu wengi hupigwa na radi na mara nyingi wanakufa.
Radi husababisha moto
kwenye nyumba au porini, ni vigumu radi kuweza kuzuiliwa kabisa, lakini madhara
yanayosababishwa na radi yanaweza kupunguzwa kwa kutumia mbinu zinazostahili.
Radi inayolenga ardhi huelekea kuingia sehemu ya juu mahali inapopiga, vifaa au
mitambo ya kikingaradi ambayo ni chuma zilizopo juu ya dari ya nyumba na
kuchimbiwa ardhini kando ya nyumba huweza kusaidia, kama radi inapiga nyumba
itachukua njia ya haraka ya kufika ardhini kwa hiyo itapita kwenye vyuma bila
kusababisha madhara kwa nyumba yenyewe.
|
Radi
zinapotokea unapaswa kuepuka vilele, kwani radi huwa na madhara makubwa
unapokuwa kileleni, kwa mfano juu ya mti, mlingoti.
Ukiwa ndani ya gari wakati
wa radi ni salama, kwani vyuma hukusaidia kukukinga dhidi ya miale ya radi na
kuelekeza ardhini. Ukiwa mahala pa wazi pasipo na kinga unaweza kuchuchumaa na
huku sehemu ya mwili ikiwa imegusa ardhi na mikono yako kati kati ya miguu.
Kamwe usiwe ndani ya maji wala kuogelea wakati wa radi kwa sababu maji ni kiungo
muhimu cha kupitisha nguvu za umeme.
|
No comments:
Post a Comment