LA LIGA 2016/2017:Real Madrid warejea Kileleni huku FC Barcelona akidundwa 2-1 na Deportivo La Coruna. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Monday, March 13, 2017

LA LIGA 2016/2017:Real Madrid warejea Kileleni huku FC Barcelona akidundwa 2-1 na Deportivo La Coruna.

Real Madrid kupitia kwa Nahodha wake Sergio Ramos Pichani akifurahia baada ya kuifungia bao la ushindi timu yake dakika ya 81 ya mchezo na kuichapa Real Betis magoli  2-1 usiku wa jana March 12, 2017 Uwanja wa Bernabeu katika mchezo wa Ligi kuu ya  La Liga 2016/2017. 

Real Betis walitangulia kwa bao la Antonio Sanabria dakika ya 24, kabla ya Cristiano Ronaldo kuisawazishia Real Madrid dakika ya 41 na kutwaa uongozi wa La Liga kutoka kwa Mahasimu wao FC Barcelona.

Mapema, Mabingwa Watetezi wa La Liga, FC Barcelona  walitandikwa bao 2-1 na Deportivo La Coruna huko Estadio Municipal de Riazor.

Deportivo La Coruna walitangulia kufunga kwa Bao la dakika ya 40 la Joselu huku Luis Suarez akaisawazishia Barcelona dakika ya 46 lakini Bergantiños García akaipa ushindi Deportivo La Coruna kwa Bao la dakika ya 74.
Kwa Matokeo hayo Real Madrid  wanaongoza La Liga wakiwa na Pointi 62 kwa mechi 26 wakifuata FC Barcelona wenye Pointi 60 kwa mechi 27 huku Deportivo La Coruna wao wapo nafasi ya 15 wakiwa na Pointi 27 kwa mechi 27.

Post Bottom Ad