Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM wapitisha mabadiliko ya Katiba ya CCM. - Mwana Wa Makonda

Breaking

Post Top Ad

Monday, March 13, 2017

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM wapitisha mabadiliko ya Katiba ya CCM.

Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dk. Joseph Magufuli akiwahutubia wajumbe wapatao 2356,ambapo walipaswa kuwa wajumbe 2380 mkutano Mkuu Maalum wa CCM ambao ulikuwa una lengo kuu la kufanya baadhi ya mabadiliko ndani ya Katiba,ambayo yamepitishwa kwa asilimia 100 na wajumbe hao waliohuhudria mkutano huo.

Wajumbe 2,356 wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Jana March 12, 2017 wamepitisha mabadiliko ya Katiba ya CCM kwa kauli moja chini ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli.

Mabadiliko hayo ya CCM yamelenga katika maeneo matatu makuu ikiwa ni pamoja na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, Kanuni za Uchaguzi za CCM pamoja na Kanuni za Jumuiya (UWT, UVCCM na Wazazi).

Mbali na hilo Mwenyekiti wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli aliweka wazi lengo kuu la mabadiliko hayo ni pamoja na kuimarisha chama chao na kukufanya kiendelee kutawala na kufanya vyema siku hadi siku.

Mabadiliko yanalenga kuboresha mfumo na muunda wa chama chetu, wa sasa una mapungufu mengi utakuta watendaji wanafanya majukumu yanayofanana na kugongana kimaamuzi, pia kuliibuka vyeo vilivyo na nguvu, watu walivitumia kwa maslahi yao binafsi japokuwa kikatiba havipo”. Alisema Magufuli

Aidha Mwenyekiti huyo alitoa onyo kali kwa mamluki yeyote atakajitokeza kuharibu mchakato huo kwa namna moja ama nyingine na kusema adhabu kali dhidi yake itachukuliwa.

Pia Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk John Magufuli amesema chama hicho hakitambembeleza mtu kukichangia katika shughuli mbalimbali na kuwa kwa miaka yote CCM kimekuwa kikiomba hata kwa watu ambao hawastahili.

Matokeo yake wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kudhalilisha. Hakuna tena omba omba hatutaki kumbembeleza mtu akitaka kutuchangia atuchangie,”amesema.

Amesema kuwa chama hicho kina utajiri unaokiwezesha kujitegemea na kwamba mwanachama atakayetumia mali za chama kwa maslahi binafsi atachukuliwa hatua kali.
 
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza mambo mbalimbali mbele ya wajumbe waliohudhuria katika Mkutano Mkuu Maalum mjini Dodoma.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana amedai kuwa kumekuwa na upotoshaji mkubwa ukiendelea kuwa mabadiliko hayo yanafanywa kwa kumlenga mtu au kundi fulani la watu na kusema huo si kweli bali wanafanya mabadiliko hayo kwa lengo la kukijenga chama.
Baadhi ya Wajumbe wa mkutano mkuu Maalum wa CCM wakishangilia kwa shangwe huku wakiwa na mabango yao yakionesha mikoa wanayoiwakilisha.

Post Bottom Ad