Nusu Fainali ya FA Cup: Chelsea v Tottenham na Arsenal v Man City. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, March 14, 2017

Nusu Fainali ya FA Cup: Chelsea v Tottenham na Arsenal v Man City.

Mourinho na Conte walikwaruzana.

Jose Mourinho amerejea tena Stamford Bridge Jijini London kwa mara ya pili akiwa Meneja wa Manchester United kuiongoza Timu yake hiyo kuikwaa timu yake ya zamani Chelsea kwenye Mechi ya Robo Fainali ya FA CUP na kujikuta wakiwa ,Mabingwa watetezi wa Kombe hilo la FA- Manchester United wakifungwa goli 1-0 na Chelsea katika mchezo huo uliyochezwa hapo Jana March 13,2017 kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

Bao pekee la ushindi kwa Chelsea lilifungwa na N'Golo Kante kwa mkwaju mkali katika dakika ya 51. 

Kadi nyekundu.

Manchester United walicheza kwa kipindi kirefu wakiwa mchezaji mmoja pungufu baada ya Ander Herera kuoneshwa kadi mbili za manjano katika dakika ya 35.

Mchezo ulibadilika baada ya Ander Herera kutolewa kwa kumchezea rafu Eden Hazard. Kipa wa United, David De Gea awali aliokoa mkwaju mkali wa Hazard. 


Mchezo huo ulighubikwa na hasira, huku Diego Costa na Marcos Rojo wakizozana mara kwa mara, wakati meneja Antonio Conte naye akikwaruzana na Jose Mourinho.


Chelsea hawakuweza kuongeza goli licha ya kupata nafasi kadhaa, Pia ni safari nyingine kwa Mourinho  anafungwa mara ya pili katika klabu yake ya zamani, baada ya kutandikwa 4-0 kaika mchezo wa Ligi Kuu mwezi Oktoba.

Chelsea watakutana na Tottenham katika mchezo wa Nusu fainali utakaochezwa tarehe 22, mwezi Aprili,2017 kwenye uwanja wa Wembley. 

Nusu fainali nyingine ni kati ya Arsenal watakaocheza na Manchester City Aprili 23,2017.
FA Cup semi-finalists recent head-to-head (previous five meetings)
Chelsea v Tottenham
1 Mar, 2015:Chelsea 2-0 TottenhamLeague Cup
29 Nov, 2015:Tottenham 0-0 ChelseaPremier League
2 May, 2016:Chelsea 2-2 TottenhamPremier League
26 Nov, 2016:Chelsea 2-1 TottenhamPremier League
4 Jan, 2017:Tottenham 2-0 ChelseaPremier League
Arsenal v Manchester City
13 Sep, 2014Arsenal 2-2 Manchester CityPremier League
18 Jan, 2015:Manchester City 0-2 ArsenalPremier League
21 Dec, 2015:Arsenal 2-1 Manchester CityPremier League
8 May, 2016:Manchester City 2-2 ArsenalPremier League
18 Dec, 2016:Manchester City 2-1 ArsenalPremier League

Post Bottom Ad