CAF yaipa Zanzibar Uanachama Kamili. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 17, 2017

CAF yaipa Zanzibar Uanachama Kamili.

      Kikosi cha Zanzibar Heroes.

Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) Jana March 16,2017 limepitisha ombi la Zanzibar kuwa mwanachama wake mpya bila ya kupingwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo uliofanyika Addis Ababa nchini Ethiopia.

Hatua hiyo inafutia maombi ya muda mrefu ya Zanzibar kutaka uanachama huo, ambapo katika mkutano mkutano huo wa Jana imekuwa ni moja ya ajenda iliyojadiliwa na kisha kupatishwa kwa kupata theluthi mbili ya idadi ya kura  wanachama wote, maamuzi ambayo sasa yanaifanya Zanzibar kutangazwa kuwa mwanachama mpya kamili wa CAF wa 55.


Mkutano Mkuu wa CAF ulipokuwa ukiendelea nchini Ethiopia jana March 16, 2017.

Uanachama huo sasa unaifanya Zanzibar iweze kushiriki michuano ya kimataifa inayoandaliwa na CAF kama taifa kamili, ikimaamisha kuwa kuanzia sasa Tanzania (Tanzania Bara na Zanzibar) itakuwa na timu mbili katika michuano yote ya CAF ikiwemo CHAN na AFCON.

Manufaa mengine ni Zanzibar sasa kushiriki Fainali za Afrika Wanawake (Awcon), Fainali za Vijana (Afcon U-17 na U-20), kuhudhuria mikutano mbalimbali kama mwanachama kamili pia kupokea na kusimamia kozi za zitakazokuwa zinatolewa CAF.

Pia Zanzibar itakuwa na fursa ya kupiga kura katika masuala muhimu ya CAF tofauti na awali ilipokuwa inapata nafasi hiyo mpaka klabu zake ziwe zimeshika nafasi ya juu katika ligi kuu Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.
Ahmed Ahmed

Katika hatua nyingine, shirikisho hilo Jana March 16,2017 limemchagua Bwana Ahmed Ahmed kutoka Madagascar kuwa Rais wake mpya, na kumbwaga kigogo katika nafasi hiyo, Issa Hayatou ambaye ndiye aliyekuwa Rais anayemaliza muda wake.

Katika uchaguzi uliofanyika kupitia mkutano huo, Ahmed amepa kura 34 dhidi ya kura 20 alizopata Issa Hayatou.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad