Zifahamu Timu 8 zilizofuzu kucheza Robo Fainali ya UEFA Europa League 2016/2017. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 17, 2017

Zifahamu Timu 8 zilizofuzu kucheza Robo Fainali ya UEFA Europa League 2016/2017.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta atacheza Robo Fainali ya UEFA Europa League 2016/2017 baada ya timu yake kufuzu licha ya kulazimishwa sare ya 1-1 na KAA Gent usiku wa jana Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.

 Kwa matokeo hayo, Genk inakwenda robo fainali kwa ushindi wa jumla wa 6-3, baada ya mwanzo kushinda 5-2 ugenini wiki iliyopita kwenye mchezo wa kwanza wa 16 Bora ikiungana na vigogo wengine wa Ulaya, wakiwemo Manchester United ya England ya kocha Mreno, Jose Mourinho.
Nao Manchester United  wameingia  robo fainali ya ya UEFA Europa League baada ya kuifunga FC Rostov  bao 1-0 katika mechi ya pili iliyochezwa Old Trafford Jijini Manchester.

Bao la ushindi la Man United lilifungwa Dakika ya 70 na Juan Mata na sasa wametinga Robo Fainali kwa Jumla ya Bao 2-1 baada ya Sare ya 1-1 kwenye Mechi ya Kwanza.
Droo ya kupanga Mechi za Robo Fainali itafanyika Saa 9 Mchana huu wa Leo Ijumaa March 17,2017 huko Nyon, Uswisi kwenye Makao Makuu ya UEFA.

Mechi za Robo Fainali zitachezwa Aprili 13 na Marudio ni Aprili 20,2017.

Robo Fainali – Timu zilizofuzu.

-Besiktas                           

-Celta Vigo

-KRC Genk

-Man United

-Schalke

-Lyon

-Anderlecht

-Ajax

Post Bottom Ad