Serikali imepiga marufuku watu kufunga ndoa bila kuwa
na cheti cha kuzaliwa kuanzia Mei Mosi, mwaka huu,2017.
Waziri wa
Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema hayo leo akiwa katika ziara
yake mkoani Morogoro na kuongeza kuwa serikali imeamua kufanya hivyo ili kupata
takwimu sahihi za wananchi wake zitakazosaidia kupanga mipango ya kimaendeleo
sanjari na kuzuia wageni kuingia kinyemela nchini.
Pamoja na
mambo mengine, Dk.Mwakyembe amewataka Wakala wa Usajili wa vizazi na Vifo
(RITA), kuhakikisha inasimamia sheria ya usajili ambapo amesema kuwa bila kuwa
na takwimu sahihi za
vizazi na vifo ama ndoa
inasababisha nchi kushindwa kusonga mbele kimaendeleo.
“Wenzetu
nchi zilizoendelea suala la usajili wamelipa kipaumbele lakini sisi bado tuko
nyuma, kwa mfano Mkoa wa Morogoro kwa
mujibu wa sensa ya watu na makazi ya
mwaka 2012, inaonyesha kuna jumla ya wakazi milioni 2.2, lakini waliosajiliwa
na kuwa na vyeti vya kuzaliwa ni
asilimia 11 pekee huku wengine wakiwa bado hawasajiliwa,” amesema.
Dk.
Mwakyembe pia ametumia nafasi hiyo kuwaonya watendaji wa mahakama
watakaolalamikiwa na wananchi kufanya kazi kinyume na maadili ikiwamo upokeaji
wa rushwa ama kutotenda haki na kutumia
mahakama kugeuza kesi za madai kuwa kesi za jinai.
|
No comments:
Post a Comment