Ingia hapa kuyaona Matokeo ya Kidato cha Nne Mwaka 2016 Yametoka. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, January 31, 2017

Ingia hapa kuyaona Matokeo ya Kidato cha Nne Mwaka 2016 Yametoka.

Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Januari 31, 2017 limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Sekondari, Kidato cha Nne kwa  mwaka 2016, mtihani ambao ulifanyika mwishoni mwa mwaka jana ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.44 ukilinganishwa na ule wa mwaka jana,2016.

Katika matokeo hayo, shule za Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam zimeonekana kung’ara zaidi kwa kushika nafasi za juu wakati huohuo  shule 6 za Dar es Salaam zikishika nafasi 10 za mwisho katika matokeo hayo.

Shule zilizoingia 10 bora Kitaifa.

  1. Feza Boys Sec School – Dar es Salaam
  2. St. Francis Girls Sec School -Mbeya
  3. Kaizirege Junior Sec School – Kagera
  4. Marian Gilrs Sec School – Pwani
  5. Marian Boys Sec School- Pwani
  6. St. Aloysius Girls Sec School – Pwani
  7. Shamsiye Boys Sec School – Dar es Salaam
  8. Anuarite Girls Sec School- Kilimanjaro
  9. Kifungilo Girls Sec School- Tanga
  10. Thomas More Machrina Sec School – Dar es Salaam
Shule za Dar es Salaam zilizoshika nafasi 10 za mwisho.

Kitonga Sec School
Nyeburu Sec School
Mbopo Sec School
Mbondole Sec School
Somangila Day Sec School
Kidete Sec School


Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26.

Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015.

Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad