WANAWAKE
NA MAENDELEO FOUNDATION
D A R ES
SALAAM | IJUMAA |DESEMBA 2, 2016
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Katika
gazeti la Raia Mwema toleo No 486 la Tarehe 30 Novemba, 2016 kumeandikwa habari
yenye kichwa kilichosomeka “Mali za Salma Kikwete kuuzwa kwa mnada?”. Katika habari hiyo kumetolewa madai ati
kwamba taasisi ya WAMA inayoongozwa na Mheshimiwa Mama Salma Kikwete inao mzigo
mkubwa bandarini ambao haujalipiwa ushuru na kodi. Na kwa sababu hiyo, Mamlaka
ya Mapato Tanzania imepanga kuuza mali hizo.
Kwa niaba ya
Taasisi ya WAMA napenda kutoa masikitiko yetu kwamba habari hizo ni za uongo na
hazina ukweli wowote.
Kwa maoni yetu gazeti hilo lina dhamira mbaya dhidi ya
Taasisi ya WAMA na Mwenyekiti wake, Mheshimiwa Mama Salma Kikwete. Nia yao ni
kupaka matope na kuchafua majina na sifa ya taasisi yetu na kiongozi wake.
Ukweli
kuhusu jambo hili ni kwamba, WAMA ilitumiwa maboksi Kumi na Moja (11) ya vitabu
vikiwa ni zawadi (grant) kutoka Nakayama Foundation ya Japani ambayo ndiyo
iliyofadhili ujenzi wa Shule ya Sekondari ya WAMA-Nakayama iliyopo Nyamisati,
Kibiti. Maboksi hayo yaliyotumwa kupitia BL 243016002211 yaliwasili bandarini
tarehe 27/06/2016.
Yalitolewa tarehe 10/8/2016 baada ya WAMA kulipia kodi zote
na ushuru wote unaotahili tarehe 26/07/2016.
Vitabu hivyo
vimekwishapelekwa shuleni na wanafunzi wanavitumia. Hakuna mzigo wowote wa
Taasisi ya WAMA uliopo bandarini unaosubiri kutolewa wala kuuzwa na TRA.
Hivyo
basi, gazeti hilo kuandika kuwepo kwa mzigo mkubwa wa WAMA bandarini ni jambo
la kughushi ambalo limefanywa kwa dhamira mbaya na kwa sababu wanazozijua wao.
Tumelitaka
gazeti la Raia Mwema limuombe radhi Mwenyekiti wa WAMA Mheshimiwa Mama Salma
Kikwete na kuiomba radhi WAMA Foundation kwa kuandika taarifa za uongo.
Gazeti
hilo limechafua sifa ya Mwenyekiti wa WAMA na WAMA Foundation kiasi ambacho
wanao wajibu wa kuomba radhi na kusafisha majina na heshima zetu mbele ya
jamii.
Ikiwa
hawatatekeleza haya ndani ya kipindi cha siku Saba, yaani kabla ya tarehe 07
Desemba, 2016, tutalazimika kuchukua hatua zipasazo za kisheria.
Daudi Nasib,
Katibu
Mtendaji,
Dar es
Salaam,
Tel: +255 22
2781287
info@wamafoundation.or.tz
|
No comments:
Post a Comment