Mkutano mkuu wa chama cha Bloggers Tanzania (TBN) Kufanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, December 02, 2016

Mkutano mkuu wa chama cha Bloggers Tanzania (TBN) Kufanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi(wa kwanza
kutoka kulia) akipokea hundi ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Ofisa  Uhusiano wa NMB, Doris Kilale kwa ajili ya kudhamini mkutano huo.

Mwenyekiti wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN), Joachim Mushi(wa pili
kutoka kulia) akipokea hundi ya shilingi milioni 10 kutoka kwa Ofisa  Uhusiano wa NMB, Doris Kilale kwa ajili ya kudhamini mkutano huo.
Mwenyekiti wa muda wa mitandao ya Kijamii Tanzania Bloggers Network (TBN), Joachim
Mushi (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano mkuu wa chama cha Bloggers Tanzania (TBN) utakaofanyika kwa siku mbili  katika ukumbi wa PSPF jijini Dar es Salaam.

Kulia ni Katibu wa  TBN,Khadija Khalili na Mwisho kushoto ni Meneja wa Mitandao wa NMB,Joyce Nsekela.

Ofisa Uhusiano wa NMB, Doris Kilale akizungumzia udhamini wa benki ya NMB  katika mkutano mkuu wa Chama cha Bloggers Tanzania (TBN) utakaofanyika  kwa siku mbili na kuwakutanisha blogger kutoka Tanzania Bara na  Visiwani.   
Akizungumza  mbele ya Wanahabari  mapema leo (hawapo pichani) ndani ya Ukumbi wa
Idara ya Habari MAELEZO,Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network  (TBN),Joachim Mushi amesema kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika  kuanzia Desemba 5 na 6 ,2016 hapa hapa jijini Dar,ambao utawashirikisha  wanachama wapatao 150 kutoka Tanzania Bara na Visiwani.Mushi alisema  kuwa katika mkutano huo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa  Habari,Michezo,Utamaduni na Sanaa Mh Nape Mosses Nnauye.


"Mgeni rasmi anaetarajiwa kufungua mkutano huo ni  Waziri Nape Nnauye,lengo  kuu la mkutano huo likiwa ni kupeana elimu na kubadilishana mawazo  juu  ya uendeshaji wa Mitandao ya Kijamii kwa manufaa,upashaji habari kwa  kutumia mitandao yao kwa kuzingatia maadili  na namna ya kunufaika na  mitandao hiyo kwa waendeshaji",alisema Mushi.


Alisema kuwa uendeshaji wa Mitandao baadhi yao wanaifanya ni kama ajira  nyingine,hivyo kimsingi lazima wakubali kuwa mitandao hii imekuwa  tegemeo kubwa la kusambaza habari mbalimbali tena kwa muda mfupi tangu  kutokea kwa tukio fulani,hivyo kuna kila sababu ya kuendelea kuwapiga
msasa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya  ya mitandao hii.



 Mkutano huo utakaokuwa wa aina yake na kuiandika historia tangu kuanza kwa  mitandano ya Kijamii hapa nchini,umedhaminiwa na Benki ya NMB ambaye ni  mdhamini mkuu ,NHIF, SBL, PSPF na Coca Cola.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad