Magari 15 yamepata Ajali na kusababisha Vifo vya Watu 17 wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 22, 2016

Magari 15 yamepata Ajali na kusababisha Vifo vya Watu 17 wilayani Ngara mkoani Kagera.

Jumla ya magari 15 yamepata ajali na kusababisha vifo vya watu 17 na majeruhi 11 katika wilaya ya ngara mkoani kagera kati ya mwezi January hadi septemba mwaka huu hali ambayo inachangia kupungua kwa nguvu kazi ya taifa. 

Mkuu wa Jeshi la polisi wilayani ngara Bw Abel Maige ametoa takwimu hizo leo,September 22,2016 wakati akizungumza na Mtandao huu kufuatia kuendelea kuwepo matukio ya ajali ya magari kuanguka na mengine kuteketea kwa moto na watu kupoteza maisha ikiwa ni pamoja na hasara kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri.


Bw Maige amesema ajali hizo zinatokea zaidi mteremko wa kasharazi,    Rusumo, Nakatunga, kumuyange, kanazi  na maeneo mengine ambapo changamoto kubwa ni madereva kutokuwepo makini na alama za usalama barabarani na kuwa na mwendo kasi.

Hata hivyo amesema mkakati wa Jeshi la Polisi wilayani Ngara ni kuweka askari wa Usalama barabarani kwenye maeneo hatarishi ambayo yamezidi kwa matukio ya ajali na kwamba wanahitajika askari watano kila kituo kukidhi mahitaji ambapo Askari waliopo ni 13 pekee wa usalama barabarani

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad