Mabingwa wa CECAFA ya Wanawake Kilimanjaro Queens yapokelewa Dar - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 22, 2016

Mabingwa wa CECAFA ya Wanawake Kilimanjaro Queens yapokelewa Dar

img-20160922-wa0036
Kilimanjaro Queens imekanyaga ardhi ya Dar ikiwa na kombe la CECAFA Women’s Championship 2016 walilolitwaa nchini Uganda kwa kuifunga timu ya taifa ya wanawake ya Kenya Harambee Starlets kwa magoli 2-1.

Timu hiyo imepeta mapokezi leo hii September 22,2016 kutoka kwa viongozi wa Serikali kupitia Wizara yenye dhamana ya michezo, Viongozi wa TFF pamoja na mashabiki ambao walijitokeza kwenye uwanja wa ndege wa Mw. JK Nyerere.
img-20160922-wa0039
img-20160922-wa0042
Safari ya Kilimanjaro Queens kuusaka ubingwa wa CECAFA Women’s Championship 2016,ilianza Septemba 9 ikiongozwa na kocha mkuu wa timu hiyo Sebastian Nkoma walikabidhiwa bendera ya taifa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera tayari kuelekea Jinja nchini Uganda baada ya kuhitimisha kambi ya siku chache mjini Bukoba.

Kabla ya kuelekea Jinja, Kilimanjaro ilicheza mchezo mmoja wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Burundi na kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0.

Wanadada hao wa Tanzania bara waliwasili Uganda wakiwa tayari kukipiga kwenye michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa wanawake katika ukanda huu wa Afrika Mashariki na Kati. Tanzania iliangukia kwenye Kundi B kundi lililokuwa na timu tatu (Tanzania, Rwanda na Ethiopia).

Ilianza kwa ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya Rwanda kisha ikatoka suluhu na Ethiopia na kufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali kwa matokeo ya kurushwa shilingi kufuatia kulingana pointi na Ethiopia.
img-20160922-wa0040

img-20160922-wa0038
Kwenye husu fainali wakakutana na wenyeji wa mashindano hayo timu ya Uganga ambapo Kilimanjaro ikafuzu hatua ya fainali kwa kuichapa Uganda kabla ya kuishinda Kenya na kutangazwa mabingwa wa CECAFA ya wanawake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad