Ligi Kuu Vodacom 2016/2017 - African Lyon yainyuka 3-1 Mbao FC na huu Ndio Msimamo wa Ligi….Utazame Hapa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, September 12, 2016

Ligi Kuu Vodacom 2016/2017 - African Lyon yainyuka 3-1 Mbao FC na huu Ndio Msimamo wa Ligi….Utazame Hapa.


Baada ya kuifunga Mtibwa Sugar Bao 2-0 za Kipindi cha Pili za mchezaji  Laudit Mavugo na Ibrahim Ajib , Simba SC wamekaa kileleni mwa Ligi Kuu Vodacom 2016/2017 pamoja na Azam FC wakifungani kwa kila kitu, wote wakiwa wamecheza Mechi 4 na wakiwa na Pointi 10 kila mmoja.
Nyuma yao wako Mabingwa,  Watetezi Yanga SC waliocheza Mechi moja pungufu na wana Pointi 7.


MSIMAMO:

NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Azam FC 4 3 1 0 7 2 5 10
2 Simba 4 3 1 0 7 2 5 10
3 Yanga 3 2 1 0 6 0 6 7
4 Mbeya City 4 2 1 1 6 3 3 7
5 Ruvu Shooting 4 2 1 1 4 3 1 7
6 Tanzania Prisons 4 2 1 1 3 2 1 7
7 Stand United 4 1 3 0 3 2 1 6
8 Kagera Sugar 4 1 3 0 1 0 1 6
9 Mtibwa Sugar 4 2 0 2 4 5 -1 6
10 Mwadui FC 4 1 1 2 3 4 -1 4
11 Toto Africans 4 1 0 3 1 3 -2 3
12 JKT Ruvu 3 0 2 1 0 1 -1 2
13 African Lyon 3 0 2 1 1 4 -3 2
14 Ndanda 4 0 2 2 2 5 -3 2
15 Mbao FC 3 0 1 2 1 5 -4 1
16 Majimaji 4 0 0 4 1 9 -8 0

Jumatatu September 12,2016,Ligi kuu Tanzania bara imeendelea kwa mchezo mmoja kati ya African Lyon dhidi ya Mbao FC mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru na Afrikca Lyon imefanikiwa kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 kwa mara ya kwanza baada ya kutoka sare katika michezo yao mitatu tangu kuanza kwa ligi msimu huu.

Mbao FC inasubiri kucheza na Ruvu Shooting kabla ya kuifuata Mtibwa Sugar Manungu Complex, Tutiani mkoani Morogoro kisha watasafiri kurejea mkoani kwao Mwanza.

Kabla ya ushindi wa leo, Lyon ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo wa kwanza wa ligi, ikafungwa 3-0 na Yanga SC halafu ikatoka 0-0 na Ruvu JKT.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad